
RAIS WA SERIKALI YA WANAFUNZI Mh NUHU SULEIMAN PAMOJA NA BARAZA LAKE LA MAWAZIRI
TAMKO LA SERIKALI YA WANACHUO
JUU YA HUDUMA ZA AFYA KATIKA ZAHANA TI YA CHUO
Ndugu CHARLES LUWONGO alijisikia vibaya na kuomba msaada chumba cha jirani mnamo saa 10:oo alifajiri siku ya tarehe 01/01/ 2010, takribani muda wa dakika mbili tayali ndugu mapunda alikua ameshafika chumbani kwa marehemu na kugundua kua alikua hayuko katika hali ya kawaida (ugonjwa) .kwakushirikiana na wanafunzi wengine ndugu mapunda walifanya jitihada za kumfikisha katika za hanati ya chuo , na kukutra imefungwa na hakuna mhudumu yeyote .Jitihada za kumpa ta dereva wa zamu katika eneo la chuo ili aweze kutoa msaada wa kumpeleka mgonjwa katika hospitali ya wilaya ya lushoto ziligonga mwamba ,kwani dereva wa zamu hakuwaepo katika eneo la chuo na simu zilikua hazipatikani .
Uamuzi ulichukuliwa wa kutembea mpaka kwa dereva anaeishi karibu na Judge kwaajiri ya kuomba msaada, walifanikiwa na kuja kumchukua mgonjwa mnamo saa 12:00 alifajiri na kumpeleka katika hospitari ya wilaya , mihangaiko yote hiyo ilichukua masaa mawili hadi mgonjwa kufika hospitari ambapo aliaga dunia hata hajapatiwa matibabu
Tukio kama hili lilitokaea kwa mwanafunzi Theresia Kinyasi mwezi mmoja uliopita ambapo baada ya kuugua ghafula mnamo ma jira ya saa 11:00 jioni alikosa huduma za usafili kwa kutokuepo dereva wa zamu na pia kukosa hudumaya matibabu baada ya kutokuwepo nesi wa zamu katika dispensary ya chuo ,na kwamba hata baada ya doktrari kupatikana alishindwa kutoa huduma yeyote hali iliyo pelekea mgonjwa kupelekea mgojwa kupelekwa hospitari ya wilaya na kupata matibabu baada ya massa mawili kupita .Huduma katika zahanati ya chuo zilikua hazilizishi siku hadi siku kwani wanafunzi wamekua wakipata usumbufu mkubwa unaotoka na uzembe wa wafanyakazi katika zahanati ya chuo , pamoja na kutokuepoeva wazamu katika eneo la chuo wakati wa usiku .
Serikali ya wanafunzi kwa kupitia wizara ya afya imekua ikifanya kazi kwa kushughulikia matatizo ya dispensary na kupeleka malalamiko kwa mshauli wawanafunzi ,pamoja na uongozi wa dispensary na kupata majibu yafuatayo ;
1)zahanati ya chuo inatakiwa kuwa wazi muda wote ili kutoa huduma kwa wanafunzi muda wowote linapotokea tatizo la ugonjwa kwa wanafunzi ,
2)kunachumba maalumu kwaajili ya dereva zamu kwaajiri ya dharula zitakazo jitokeza.
Kwa kuwa Majibu hayo yamekuwa yakikinzana na hali halisi ,Hivyo kupelekea usumbufu mkubwa wanafunzi wanaopata ya ugonjwa hususani wakati wa usiku ,na kwakuwa mfano hai tumeupata kwani marehemu Ndugu Charles Luwongo hakupata huduma yoyote ya kwanza kutokana na kufungwa kwa Zahanati ya Chuo mpaka anafika katika hospitali ya Wilaya , na kwa kuwa ugonjwa hauchagui kwani hatujui leo au kesho ataugua nani ,na kwa kuwa miongoni mwetu kuna baadhi ya wanafunzi wenye magonjwa ya dharura kama vile moyo, Athma , kisukari, n.k. Serikali ya wanafunzi inaomba Utawala wa Chuo uchukue hatua zifuatazo;
1. Kutokana na kukosekana / kufungwa Zahanati ya Chuo mara kwa mara , mfano siku ya mkesha wa mwaka mpya ; siku ambayo ata Taifa linatambua umuhimu wake kwa ongozeko la matukio na hivyo kuimarisha usalama wa watu wake katika Nyanja mbalimbali , Utawala wa Chuo uchukue hatua za kinidhamu kwa mamlaka na watu husika waliopelekwa kufungwa kwa Zahanati na kukosekana kwa Zahanati na kukosekana kwa dereva wa zamu katika siku hiyo muhimu.
. 2. Utawala wa Chuo utoe tamko la kulaani tukio lilitokea siku ya mkesha wa
waka mpya hususani ukosefu wa huduma za Zahanati na dereva wa.
Zamu.Tamko hilo liwahakikishie wanafunzi usalama wa afya zao
Kuhakikisaha upatikanaji wa huduma bora za afya , pamoja na kuwepo na
Daktari au nesi muda wote ; sambamba na upatikanaji wa dereva wa zamu
Katika eneo la Chuo wakati wa usiku.
3. Kutokana na kuzorota kwa huduma za Zahanati ya Chuo, Utawala wa Chuo uchukue hatua za haraka ili kunusuru hali hii . Na kama haiwezekani wanafunzi warudishiwe fedha zao wanazotoa kwa ajili ya matibabu ili waweze kujihudumia wenyewe kw uhakika.
Ili matatizo tuliyoyaanisha hapo juu yapewe umuhimu na kushughurikiwa haraka iwezekanavyo kwa manufaa ya wanafunzi wote , Serikali ya wanafunzi inatoa tamko la kususia, vipindi madarasani ( Boycott classes) kuanzia leo tarehe 04/01/2010 kama njia pekee ya kikatiba ya kushinikiza Utawala wa Chuo kutatua matatizo yanayotukabili. Tunategemea kupata majibu ndani ya masaa 48 kuanzia sasa, na ikishindikana ndani ya muda husika Serikali ya wanafunzi itachukua hatua zaidi.

MWILI WA MAREHEM CHARLES UKITOREWA NDANI YA UKUMBI WA NYALALI SQURE KWAAJIRI YA KUSAFILISHWA KWAO

No comments:
Post a Comment